Hata Raila Odinga anapozunguka nchi nzima akijaribu kuwashawishi Wakenya kuungana naye Jumatatu, Machi 20, 2023 katika kumtuma nyumbani rais Ruto, kuna jambo muhimu sana anasahau kufanya.

Kiongozi huyo wa upinzani anaangazia zaidi watu wasiomuunga mkono huku akisahau chama chake cha ODM ambacho kinakaribia kusambaratika.
Odinga amekuwa akipokea vita baridi kutoka kwa baadhi ya wanachama wakuu na washirika wa ODM ambao wameamua kumegemea rais William Ruto.
Mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor ni miongoni mwa viongozi ambao wamejitenga na mpango wa Raila.
Viongozi hao, wakizungumza katika majengo ya bunge walisema kuwa hawatakuwa popote karibu na hatua ya Raila Odinga Jumatatu, wakidai kuwa ni kinyume cha sheria.
“Tunaamini kwa dhati kwamba changamoto za sasa za kiuchumi za Kenya hazitatatuliwa kwa makabiliano ya kisiasa na aina nyinginezo za ushabiki wa kisiasa.
“Ni wakati wa kuwa na Mazungumzo ya Kitaifa ya Kiuchumi kutafuta suluhu kwa changamoto zetu za pamoja za kiuchumi. Ushindani wetu wa kisiasa uwe katika kiwango cha kushindana kwa mawazo ya kiuchumi,” viongozi hao walisema kwenye taarifa ambayo ilikuwa tayari na Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi.
“Tunawasihi wapiga kura wetu kufanya vivyo hivyo. Acha ushindani wetu wa kisiasa uwe katika kiwango cha mawazo pinzani ya kiuchumi,” waliongeza.
Wabunge hao ni pamoja na; Gideon Ochanda (Bondo), Mark Nyamita (Uriri), Caroli Omondi (Suba Kusini), Paul Abuor (Rongo), Elisha Odhiambo (Gem), Phelix ‘Jalang’o’ Odiwuor (Lang’ata) na Seneta Tom Ojienda (Kisumu. More


One thought on “Jambo la kushangaza Jalang’o alimwambia Raila Odinga kabla ya Maandamano ya siku ya Jumatatu!”
Comments are closed.