Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) mnamo Jumatatu, Machi 13 alitangaza kwamba mashtaka yote dhidi ya aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Fred Matiang’i na Wakili wake Dunstan Omari yametupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi wa kutosha.

“Ushahidi uliotolewa haukukidhi viambajengo vinavyohitajika kuthibitisha kila kosa lililotajwa kama inavyotakiwa kisheria.
“Mkurugenzi wa Mashtaka kwa hivyo ameiagiza Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai kufunga faili ya uchunguzi bila hatua zozote za polisi,” taarifa ya ODPP ilisoma kwa sehemu.
Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) ilikuwa imemshtaki Matiang’i kwa njama ya kutenda jinai na kuchapisha taarifa za uongo.
Haya yanajiri saa chache baada ya Waziri huyo wa zamani kuwa na mkutano wa faragha na waziri wa elimu Ezekiel Machogu huko Karen.
Tetesi zinasema kuwa, Fred Matiang’i amekubali kujiunga na kufanya kazi na serikali ya Kenya Kwanza kwa ajili ya maendeleo ya ardhi ya Gusii. More


2 thoughts on “Imefichuliwa; Mbona DPP ametupilia mbali kesi ya Matiang’i baada ya kukutana kwa siri na waziri wa Ruto!”
Comments are closed.