Wakenya walioko Tanzania wahimizwa kuwa makini kufuatia onyo la maandamano mapya

Dar es Salaam, Tanzania – Ubalozi wa Kenya nchini Tanzania umewataka Wakenya kuwa makini na kuchukua tahadhari kutokana na ripoti za uwezekano wa machafuko wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru tarehe 9 Desemba 2025.

Picha ikionyesha maandamano tanzania

Kwenye taarifa iliyotolewa Ijumaa, Desemba 5, Ubalozi umewahimiza raia wake walioko Tanzania kubaki ndani ya nyumba iwapo kutatokea machafuko na kuepuka kusafiri au kufanya shughuli zisizo za lazima.

Pia Wakenya walipewa ushauri wa kuepuka mikusanyiko mikubwa, maandamano, na maeneo yenye usalama mkali. “Hali inaweza kubadilika haraka, hivyo fuateni taarifa rasmi pekee,” taarifa hiyo ilisoma.

Ubalozi uliwahimiza pia raia wake kuwa na mpango wa mawasiliano na familia na marafiki, ikizingatiwa uwezekano wa kukatika kwa huduma za intaneti na simu. Walisihi pia kuhakikisha wanayo chakula, maji, dawa muhimu, na simu zilizo tayari kwa kutumia.

Kwa wale wanaohitaji msaada au huduma za kisheria za dharura, Ubalozi umewaambia Wakenya kuwasiliana kupitia namba [+255-690-283-011 au +255-690-283-012] au barua pepe kwa daressalaam@mfa.go.ke.

Facebook Comments Box

Next Post

ODM Yataka majadiliano mapya na Rais Ruto kabla ya 2027!

Sun Dec 21 , 2025
Viongozi wa chama cha ODM wameendelea kushinikiza majadiliano mapya kuhusu uhusiano wao wa kisiasa na chama tawala cha UDA kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027. Wakizungumza katika eneo bunge la lugari kaunti ya kakamega nyumbani kwa aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Cyrus Jirongo aliyeaga dunia, Mwenyekiti wa kitaifa wa ODM […]

You May Like