Sio Uhuru- Raila Odinga afichua chanzo cha fedha katika maandamano ya Azimio!

1

Kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja one Kenya Raila Odinga amefichua ni nani anafadhili mikutano na demos inayoendelea ya Azimio.

Kiongozi huyo wa upinzani alipuuzilia mbali madai kwamba maandamano na mikutano yake dhidi ya serikali inafadhiliwa na aliyekuwa mkuu wa taifa Uhuru Kenyatta.

Katika mahojiano na shirika la kitaifa la vyombo vya habari, Raila alidokeza kuwa mabaraza ya umma na shughuli nyingi zinazosubiriwa zinafadhiliwa na wananchi kikamilifu.

Waziri mkuu huyo wa zamani alifichua kuwa wanachama wa muungano wa Azimio huchangisha fedha kwa hiari kwa shughuli za chama.

Waziri mkuu huyo wa zamani alifichua kuwa wanachama wa muungano wa Azimio huchangisha fedha kwa hiari kwa shughuli za chama.

Raila aliendelea kumkomboa rais wa zamani Uhuru Kenyatta kutoka kwa lawama kwamba yeye ndiye anayefadhili mikutano ya Azimio na demos.

“Hii maandamano haijagharamiwa na mtu yoyote, wananchi wenyewe ndio wanafund. Hakuna mtu anaweza kuwa na pesa kiasi cha kufund hii maandamano.

“Sisi wenyewe tunachanga hapa na pale kugharamia hii maandamano Sisi ni harakati ya wananchi” Raila alisema.

Ufafanuzi wa Raila unajiri siku chache baada ya naibu wa rais Rigathi Gachagua na washirika wake kumshutumu aliyekuwa mkuu wa serikali anayefadhili muungano unaoongozwa na Raila kufanya maandamano hayo makubwa.

“Hawa wanaomfadhili huyu mzee waache kuishi kwa kukataa…huyu mzee alipotea…hakuna wanachoweza kufanya,” alisema DP.

Facebook Comments Box

One thought on “Sio Uhuru- Raila Odinga afichua chanzo cha fedha katika maandamano ya Azimio!”

Comments are closed.

Next Post

SG wa ODM Edwin Sifuna afichua maelezo machafu kuhusu hatua ya kesho, Raila akasirishwa!

Sun Mar 19 , 2023
Katibu mkuu wa chama cha Orange Democratic, Edwin Sifuna amewaonya watu watakaohudhuria hafla ya Azimio iliyopangwa , kuwa tayari kwa mambo mabaya na mabaya. Katika maandamano yaliyopangwa ya Raila, ambayo wanaamini ni ukombozi, Sifuna alidokeza kuwa katika harakati zozote za kulikomboa taifa baadhi ya usumbufu na usumbufu hutokea katika mchakato […]

You May Like