Raila atoa sababu kuu ya kutangaza maandamano ya kitaifa!

3

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga siku ya Alhamisi alisema kua ametangaza maandamano kote nchini baada ya muda wa siku kumi na nne ambao alimpa rais William Ruto kuisha.

Raila Odinga

Akizungumza baada ya kikao na wana Azimio la Umoja One Kenya, Kinara huyo wa ODM alisema William Ruto hakutilia matakwa yake maanani akisema hakuna jambo Ruto amefanya tangu achaguliwe kua rais watano wa nchi.

Odinga pia alizindua vuguvugu la Movement for Defence of Democracy (MDD) alilosema litaendesha shughuli za kukomboa wakenya kutoka uongozi wa kiimla na usiojali maslahi ya wananchi.

“Tumeanzisha kampeni ya kwenda maandamano ya amani, kususia, kutotii na kuandamana,” Raila alisema. More

Facebook Comments Box

Next Post

Karen Nyamu kuwania kiti cha ugavana wa Nairobi na kuteuwa Samidoh kama naibu wake

Fri Mar 10 , 2023
Seneta mteuliwa wa Nairobi Karen Nyamu ametangaza njama yake ya kuwania kiti cha ugavana wa jiji la Nairobi Mwaka wa 2027. Kupitia mtandao wa Facebook, Nyamu aliweka picha yake ambayo alipigwa akiwa amesimama kwenye ofisi ya gavana wa Nairobi na kuambatanisha na ujumbe ulioashiria anatazamia kuchukua wadhifa huo siku moja. […]

You May Like