Gachagua afichua jinsi alivyomdanganya Kindiki kumwacha awe mgombea mwenza wa Ruto baada ya kufungiwa chumbani!

3

Aliyekuwa mbunge wa Mathira ambaye sasa ni naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua siku ya Jumapili aliwaacha Wakenya kwa mshangao.

Gachagua, Kindiki

Hii ni baada ya kufichua jinsi alivyomhadaa Waziri wa Mambo ya Ndani Abraham Kithure Kindiki kumwacha awe mgombea mwenza wa Ruto.

Akizungumza katika Kaunti ya Tharaka Nithi baada ya kuhudhuria ibada ya shukrani ya kanisa la Gavana Muthomi Njuki akiwa na Ruto na viongozi wengine, Gachagua alisema kuwa Ruto alikuwa na wakati mgumu kuchagua kati ya wawili hao.

Kulingana na Gachagua, Ruto alitumia saa nyingi kujaribu kubaini ni nani alikuwa bora kati ya wawili hao kwa kuwa wote walikuwa viongozi wa kutumainiwa na mashuhuri.

“Rais alikuwa akijaribu kufanya uamuzi kwa saa 17 na ikatua kwa Kindiki na mimi mwenyewe. Niko kamili, yuko kamili, ninaaminika, na yeye pia,” alisema Gachagua.

Kamanda wa pili alisema ilimbidi kumshawishi Kindiki kuwa ni mdogo kwake na hivyo ilimbidi amheshimu na kumwacha achukue wadhifa wa mgombea mwenza wa Ruto, akiongeza kuwa aliahidi pia kumtuza afisi yenye nguvu.

“Ruto alituambia tukae chini tuzungumze.

“Niliapa kumzawadia ofisi yenye nguvu, na haikufanyika? Na mimi nakushauri wewe (Kindiki) ushirikiane kwa karibu na Rais na mimi mwenyewe kwa sababu maisha yako ya baadaye ni mazuri,” alisema. More

Facebook Comments Box

Next Post

Imefichuliwa; Mbona DPP ametupilia mbali kesi ya Matiang'i baada ya kukutana kwa siri na waziri wa Ruto!

Mon Mar 13 , 2023
DPP: Matiang'i hana kesi ya kujibu

You May Like