Viongozi wa chama cha ODM wameendelea kushinikiza majadiliano mapya kuhusu uhusiano wao wa kisiasa na chama tawala cha UDA kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.

Wakizungumza katika eneo bunge la lugari kaunti ya kakamega nyumbani kwa aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Cyrus Jirongo aliyeaga dunia, Mwenyekiti wa kitaifa wa ODM ambaye pia ni gavana wa kaunti ya Homabay Gladys Wanga na mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed, wamesema mgao ambao walipata kwenye serikali jumuishi ya broadbased hautoshi.
Wanasema ili kumuunga mkono rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu wa 2027, itabidi wajadili upya mgao wa ODM..
Naye naibu kinara wa chama hicho Godfrey Osotsi alisisitiza kwamba wanataka serikali itekeleze ajenda 10 walizokubaliana,.
Facebook Comments Box
