Gavana wa kaunti ya Kakamega Fernandes Barasa sasa anaitaka serikali ya kitaifa kuinglia kati na kumaliza mzozo kuhusu kugatuliwa kwa sekta ya afya nchini.

Akizungumza katika uzinduzi wa hazina maalum ya huduma za afya katika uwanja wa Bukhungu, gavana Barasa amesema magavana wote 47 nchini wanatarajia serikali ya kitaifa kuwaunga mkono katika juhudi za kuimarisha sekta hiyo ya afya ambayo inakumbwa na changamoto si haba.
Naye naibu wa gavana wa kaunti hiyo Ayub Savula ambaye alihudhuria uzinduzi huo ameitaka wizara ya afya kushughulikia mgogoro kuhusu kadi za NHIF akisistiza kuwa wagonjwa wananyimwa huduma katika hospitali za kibinafsi kwa kuwa hospitali hizo hazijapokea malipo kutoka kwa hazina ya kitaifa ya bima ya afya.
Hafla hiyo ambayo inatarajiwa kuimarisha huduma za afya katika kaunti ya Kakamega, ilihudhuriwa na katibu mkuu katika wizara ya afya Harry Kimutai ambaye amehakikisha kuwa serikali kuu imejitolea kuona kwamba sekta ya afya nchini inaimarishwa.

