Mwili wa mwanamume huyo ulipatikana ukining’inia kwenye kamba iliyofungwa kwenye boriti ya paa.

Kulingana na chifu wa Kiarukungu Henry Kariuki, mwanamume huyo alikuwa amemtembelea afisi yake kulalamikia kisa hicho, lakini hakujua mwanamume huyo alikuwa katika hali mbaya kiakili na angejitoa uhai.
Kariuki alisema mnamo Jumatano, alimvamia mkewe kwa panga na akakimbizwa hospitalini ambapo alitibiwa na kuruhusiwa.
“Kesi hiyo iliripotiwa katika kituo cha polisi cha Wang’uru,” Kariuki alisema.
Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Mwea Mashariki Daniel Kitavi alisema marehemu alitarajiwa kurekodi taarifa kuhusu shambulio hilo, lakini akapatikana amefariki.
“Baadhi ya mashahidi waliomwona akimshambulia mkewe wamerekodi taarifa,” Kitavi alisema.
Kulingana na chifu wa Kiarukungu, mwanamume huyo alionekana mwenye msongo wa mawazo kutokana na madai ya mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kijana huyo aliyekuwa akiuza nyanya kijijini humo.
“Hatukufikiri mambo yangeisha hivi kwa sababu alikuwa amesema ameamua kuwaacha wawili hao kufanya walivyotaka,” Kariuki alisema.
Kaka wa marehemu alisema, “Alishtuka baada ya kukuta mke wake alikuwa kwenye mapenzi na mwanaume mdogo kuliko mwanawe.”
Wanakijiji walionyesha mshtuko, wakisema mwanamume huyo alipaswa kuacha mambo yaende na kuendelea. More

