Seneta mteuliwa wa Nairobi Karen Nyamu ametangaza njama yake ya kuwania kiti cha ugavana wa jiji la Nairobi Mwaka wa 2027.

Kupitia mtandao wa Facebook, Nyamu aliweka picha yake ambayo alipigwa akiwa amesimama kwenye ofisi ya gavana wa Nairobi na kuambatanisha na ujumbe ulioashiria anatazamia kuchukua wadhifa huo siku moja.
“Kanairo ipo siku! Habari ya asubuhi,” Karen Nyamu aliandika.
Kati ya watu ambao walichangia katika picha hiyo ya Nyamu ni ikiwemo aliyekua gavana wa Nairobi Mike Sonko ambaye alimkejeli Nyamu kwa kumwambie achukue Samidoh kama muwania mwenza ili Nairobi iwe county ya ‘Mugithi’.
“Ndio, na Samidoh akuwe naibu wako ikue kanairo ya Mugithi,” alimwambia.
Hata hivyo, Karen hakumjibu gavana huyo wa zamani, ila baadhi ya wafuasi wake wengine pia walimtia moyo kupigania nafasi hiyo ya uongozi siku za usoni huku wengine wakimkatiza tamaa kwa kumwambia hawezi. More

